Friday, September 10, 2010

MSEMO! MSEMO ! MSEMO NO. 2

(Kwa nini Wanuna? / Raha jipe mwenyewe)
(KWA YESU HAKUNA KUNUNA KUNA RAHA YA AJABU HEBU MKARIBISHE KWENYE MAISHA YAKO UONJE RAHA YAKE. WAKATI WOTE NI FURAHA, AMANI UPENDO KICHEKO KAZI YETU NI KUUNGANA NA MASERAFI NA MAKERUBI, WAZEE 24 NA WENYE UHAI WANNE TUNASIFU NA KUIMBA MTAKATIFU! MTAKATIFU! MTAKATIFU HAKUNA KUCHOKA HAKUNA KULALA TUMEJAA NGUVU TUNA AMANI TUNAYE BABA MWENYE UWEZA WOTE kwa nini tununeeeeeeeee tunacheza tu tunarusha taji tunadaka tunaima tunainuka usiku na mchana kazi yetu moja kusiffuuuuu wajua siri ya kusifuuu. YESU NI BWANA

MSEMO, MSEMO, MSEMOOOOO NO:1

(Waswahili wanasema Mpende Akupendaye Asiyekupenda Achana Naye) Lakini Biblia inasemaaaa MPENDE AKUPENDAYE, MPENDE ASIYEKUPENDA MPENDE, ADUI YAKO TENA KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE. Mpendwa umeikubali hiiiiiiiii
JAMANI KWA YESU KUNA RAHAAAAAAAAAAAAA; TUDUMISHE UPENDO

MISEMO

NDUGU ZANGU WAPENZI KATIKA BWANA NAWASALIMU HABARI ZETU, BWANA APEWE SIFA. NILIWAAHIDI KUWA NITAWAPA MISEMO,JE WAJUAAAA? (mambo ambayo hukuwahi kusikia hapo kwanza au ndio mara ya kwanza kusikia kuhusu Biblia) VIONJO NA MANJONJO MENGINE KIBAO KUTOKA KWENYE BIBLIA YETU. NENO LA MUNGU LINAUTOSHELEVU WOTE HAKUNA KITU KIMEACHWA BWANA TENA KATIKA ULIMWENGU WETU HUU TUNAOISHI LINAFANYA KAZI. KARIBU MTUMIE NA MWENZIO

UPENDO WA KWELI

Bwana Yesu Apewe Sifa! Namshukuru Mungu sana kwa wema na fadhili zake anazonitendea siku hadi siku, nimeuona wema, uweza na upendo wake kwangu kila iitwapo leo. Nalitukuza jina lake na kumwinua maana hakika anastahili kuinuliwa, kupewa sifa na hata kusujudiwa. Tumwamini maana yeye ni mwaminifu na ahadi zake ni kweli. Soma Warumi 4:20-21
Upendo wa KINDUGU (UPENDO WA AGAPE) Jamani tuwe na pendo/ penzi la kweli sisi tulio waaminio. Tupendane sisi kwa sisi kama Mungu alivyotupenda hata akamtoa MWANA WAKE WA PEKEE YESU AFE msalabani kwa ajili ya dhambi zangu mimi na wewe. Soma Warumi 5:8 Mungu ametupenda upeo jamani haijalishi umefanya dhambi kiasi gani, haijalishi umemkosea mara ngapi, haijalishi kama umeokoka ukakengeuka ukarudi nyuma , haijalishi umeokoka au haujaokoka bado ANAKUPENDA tena kupitiliza UPEO!! (anasema nawanyeshea mvua wema na waovu) Mbona na sisi tusipendane? Kwa maana tumeshaunganishwa na kuwa wandugu kupitia mwana wake Yesu Kristo. Tena tunaitwa watoto wa Mungu? soma Warumi 8:16 tumebeba sura na mfano wake yeye aliyetuumba, je tabia zake tunazo au tumeziacha wapi wapendwa kwa maana tabia ya Mungu ni ya Upendo na anataka TUPENDANE na amri Kuu Yesu aliyotuachia ni UPENDO. Kwanini tusipendane basi, tusiwe wamoja tusilie nao waliao na tucheke na wachekao? kwa nini tuwe wanafiki? kwa nini hatufurahishwi na mwenzetu akipata mafanikio au hata anapobarikiwa? Kwa nini uwe na upendo na mtu kwa vile unapata kitu fulani kutoka kwake kama hakuna basi huna time naye? Wivu wa nini? wakati sisi wote ni wana wa Mfalme tena Mfalme wa Wafalme.
Nasema hivii Wivu hauna nafasi tena katika jina la Yesu, Upendo wa kinafki naukataa katika jina la Yesu, Roho ya korosho ndio naifunga na kazi zake zote ktk Jina la Yesu, husuda naifunga nakuitupa kuzimu katika jina la Yesu Kristo aliye hai. Nakataa Roho zote hizo zinazofanya wana wa Mungu  tusipendane. Nafunga mipango yote na hila alizopanga mwovu shetani kwa ajili ya wana wa Mungu wasiwe na Upendo. Naambukiza Upendo wa kweli wa AGAPE utokao kwa Baba na Bwana wetu Yesu Kristo. Amen Amen.
Biblia inasema kuwa Mungu alitupenda upeo yaani alitupenda kupitiliza hakuna ukomo ktk penzi lake kwani yeye ni Mungu wa Upendo hata tunapokuwa kwenye upendo huu tunaweza kubomoa na kuangusha kuta zilizotuzingira. Kwenye UPENDO basi amani, furaha, ujasiri, neema lazima vipo na sehemu hiyo ujue kuwa Utukufu wa Mungu upo, Yesu yupo na Roho Mt yupo na yule mshitaki wetu shetani hana nafasi mahali hapa kabisaaaa.
Kama wewe unasema kuwa umeokoka na hauna Upendo basi ujue unajidanganya bado haujaokoka kwani hata Bibilia inakukataa kuwa wewe si wa Mungu Soma 1Yohana 4:8; 1Yohana 4: 16b. Ndugu yetu Petro anasema kuwa "Tuwe na juhudi nyingi ktk KUPENDANA kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi" Soma 1Petro 4:8 ina maana kwamba ukiwa na upendo wa kweli hutaweza kumbagua mwenzako kwa kuangalia sura, mavazi, fedha, mali nk wala kumdharau bali utampenda kama jinsi alivyo hutakuwa na kijicho pembe kwa mafanikio yake ya Kiroho na ya kimwili pia, bali utafurahi naye na kuhuzunika naye pale apatwapo na msiba (siyo kifo msiba lina maana mbili)
"KILA AMCHUKIAYE NDUGU YAKE NI MWUAJI, na mnajua kuwa KILA MWUAJI HANA UZIMA WA MILELE. TUSIPENDE KWA NENO, WALA ULIMI BALI KWA TENDO NA KWELI" Haya si maneno yangu bali yatoka kwenye Bibilia. Kwenye upendo jamani Hofu haina nafasi Paul anasema hivii "KATIKA PENDO HAKUNA HOFU, LAKINI PENDO LILILOKAMILI HULITUPILIA NJE HOFU, KWA MAANA HOFU INA ADHABU, NA MWENYE HOFU HAKUKAMILISHWA KATIKA PENDO" haya kama una hofu ikatae haraka sana ktk JINA LA YESU. Upendo utokao kumoyo wapendwa ambayo ndiyo tabia ya baba yetu. (kama mataifa wanaweza kumpenda mtu jinsi alivyo iweje sisi tuliopata neema ya uokovu tushindwe???? ( NANUKUU WIMBO WA DUDU BAYA "Nakupenda tu vile ulivyo nakupenda tu PUA KAMA ANDAZI NAKUPENDA TU ) sisi je haitupasi kuwa na UPENDO WA KWELI!!!!! kwenye Upendo pia kuna Umoja wapendwa na kwenye Umoja kuna nguvu ya ajabu ambayo Mungu anaiachilia, na yeye mwenyewe hushuka watu wakiwa na umoja na wakishikana SOMA 2M/Nyakati 5:13-14 "quote walipokuwa kama mmoja " (sehemu nyingine Mungu pia anaogopa Umoja jamani ndio maana hata wanadamu walipodhamiria kwa umoja kutaka kujenga Mnara wa Babel aliwatawanya kwa kuwapa lugha tofauti sababu ya nini NGUVU ILIPYOPO KWENYE UMOJA na umoja wa kweli hutoka kwenye "UPENDO WA KWELI. Tupendane sisi kwa sisi, upendo wa Agape, Upendo ambao Yesu alituachia kama AMRI KUU YA KUPENDANA. Kwani tukipendana tutashikana, tutashirikiana tutakuwa mamoja na kunena lugha moja na kumpenda Mungu kwa kulisoma NENO lake na kutenda huu ndio UPENDO autakao kwetu. UPENDO! UPENDO! UPENDO nitaendelea siku nyingine huu ni utangulizi somo lipo kuuubwa!bado hata sijaanza subiri uhondo misemo ya kwenye biblia na mistari ya kukufundisha.
SOMA 1Yohana wa Kwanza, wa Pili na Tatu Yote Kwa habari ya Upendo. Kuhusu ujenzi wa mnara (Babeli) soma Mwanzo 11:1-9