Saturday, October 16, 2010

WAMEJAA TUMAINI NA WANAAMANI No. 3

Wanafuraha ya ajabu hawana mawazo wanaamani haijalishi hali ngumu kiasi gani ya maisha wanapitia burudani lazima iwepo. Tuweni kama watoto wadogo jamani hata biblia yetu inatuambia.


VAZI LA KWENDEA KANISANI

Haya wapendwa ahadi ni deni vivazi hivi hapanaaaa vya kanisani (hebu piga picha umekaa mbele na kivazi hizi inakuwaje jamani) mkao utakavyokuwa unahangaika haya mara Roho Mtakatifu anakushukia si ndio kazi itakuwa kweli kweli kwa maana itabaidi wamama wawe na kazi ya ziada ya kukufunika kila wakati. Tujiangalie na vivazi vya kuendea kanisani.

Hivi ni vitenge lakini mashono yake ni mazuri ila si kama tulivyozoea kuburuzaa yanafaa sehemu nyingine lakini si kanisani.

Sisteri naye kapendeza lakini bado kuendea kanisani itakuwa kwazo kwa wengine. Alau ifike kwenye magoti hivi japo kwa wengine bado ni kikwazo lakini ni heri kuliko cha juu juu namna hii ingawa ndio design yake.


















.
Bibie kapendeza kweli lakini kanisani nooo big noooo. Nayo kama ya hapo juu ingefika kunako kwenye magoti ingependeza zaidi kwa mtoko wa kanisani.

VAZI LIFAALO BASI TUANGALIE ANGALAU UKIKAA AKHA MWENYEWE UNAJIACHIA NO FEAR NO MASHAKA MASHAKA.


Hapa ya bluu ndio azima yangu haswa kwa wale kama mimi tusiopenda kubaanwa na manguo ni nzuri na kuburuza ndio huko ila hii hata ikifika kunako magoti sio mbaya sana jamani au mwasemaje

Hii ni nzuri kiasi chake si mbaya japo imekaa mkao fulani hivi lakini kwa masister du si mbaya kwani aweza jirusha bila taabu.

Ukiacha hayo makofia kwa maana mengine ni makubwaa hata ukikaa mbele mwenzio unakuwa unamziba otherwise kwa kanisani nguo hizi ni bomba sana bila hiyana mtoto wa kiafrica unatoka chicha.








African touch : mwawaona mamas wakiafricaaaaa?

more pict to come.........
(Kwa hisani ya Zeze na The light)

AM BACK

BWANA APEWE SIFA SANA SANA!

POLENI SANA NDUGU WAPENDWA MAMBO MENGI KIDOGO ILA NIMERUDI NA NGUVU ZOTE NA UPAKO WA ROHO MTAKATIFU. KAENI MKAO WA KULA CHAKULA CHA UZIMA. KWA WALE MLIONITUMIA E-MAIL KUNIAMBIA KULIKONI MBONA KIMYAAA SASA NIMEREJEA. KARIBU SANA NA MBARIKIWE NA BWANA YESU ALIYE HAI.