Friday, October 29, 2010

KIU YA NENO

MIKA 7:6B ADUI WA MTU NI WATU WA NYUMBANI MWAKE MWENYEWE.

Nilikuwa nasoma Neno la Mungu nikafika kwenye kitabu cha Mika nikakutana na hili mimi mwanzo nilidhani ni mithali ya kiswahili tu kumbe ni Neno lililopo kwenye Biblia. Kusema kweli tunapoambiwa kuwa hii Bibilia ni mpya kila siku tusishangae kwani unaweza ukawa umesoma mara mia lakini kila unaporudia kusoma lazima ukutane na jambo jipya.
Kumbe adui yako hatoki mbali ni yule yule unayekula naye na kucheka naye na kulala naye. Ndio hata tunaambiwa kuwa mchawi halogi (hamchawii) mtu ambaye hamjui huwa mara nyingi anahangaika na wale awajuaye. Mara nyingi adui zetu wanakuwa ni ndugu, jamaa au marafiki zetu wa karibu ndio wanaokuwa wabaya zetu kwani anakujua vizuri jina lako, la baba yako la utotoni unavyokula unavyolala na hata siri za ndani ya nyumba zetu wanazijua. Hivyo inakuwa rahisi kwao kuchezea maisha yetu bila mpango, mara nyingi inakuwa ni husuda tu, chuki binafsi na mambo mengine kama hayo.
Lakini hii yote inatokana na Nini? Kumkosa Yesu katika maisha yao ndiko kunakowafanya watu wa jinsi hii kuanza kuwatenda mwenzao mambo yasiyofaa kuwa na chuki na husuda juu ya maisha ya wengine. Watu kama hawa hawataki kabisa kuona watu wana amani, furaha, maendeleo katika maisha yao, hivyo wanajitahidi kwa kila namna na jinsi ili uweze kuteseka kwani wao wameshakuwa ni wafuasi wa yule ibilisi. Kufanya mambo kama hayo kunawapa burudiko fulani ambalo ni la muda mfupi ambapo wanafurahia sana wanapoona umeanguka, umerudi nyuma kimaendeleo, watoto wako wanapokuwa mwiba ndani maisha yako n.k. Cha msingi ni kuwaombea kwa Mungu ili awarehemu na awasamehe na pia wapate ukombozi wawe na hofu ya Mungu kusudi watoke katika hivi vifungo. Ukisoma Galatia 5:19-21 utaona vifungo vilivyowakalia watu ambapo ni maombi tu yanahitajika mtu anakuwa huru.
Cha kufanya sisi wana wa Mungu ni kumkubali Yesu kuwa ni Bwana na Mokozi wa maisha yetu kiukweli kweli kutoka moyoni si maneno matupu, kuwa na kiu ya kusoma Neno la Mungu, kuliishi Neno kwa maana ya kulitendea kazi Neno tunalosoma na Imani yetu kwa Mungu. Kwani ukimwamini Mungu kuwa yeye anaweza kukushindia kila jambo ndani ya maisha yako hata hao adui zako kama ni wachawi au unenewe maneno mabaya kiasi gani, majaribu yawaye yote hayatakutikisa wala kufanya kazi (hayatatendeka) ndani ya maisha yako, wala kwa familia yako au wanao, kazi, afya yako n.k.Utaishi kwa amani, furaha na utaona baraka zotee Mungu alizotuahidia katika maisha yetu zikitimilika kwako. Biblia inasema ktk Mika 7:8 hata ukikaa gizanii Bwana atakuwa NURU kwako. NA BWANA WETU YESU KRISTO ANATUAMBIA MANENO HAYA PIA KATIKA YOHANA 8:12 MIMI NDIMI NURU YA ULIMWENGU, YEYE ANIFUTAYE HATAKWENDA GIZANI KWAMWE, BALI ATAKUWA NA NURU YA UZIMA.
Tusitembee gizani tena, tusitembee tukiwa tumesononeka tena, tusitembee tukiwa na hofu na mashaka juu ya adui zetu tena, tusilie vitandani mwetu tena kutokana na mateso ya magonjwa, uchungu nk kwani tunaye aliyejitolea kuyabeba hayo yote na kututoa katika shida hizo zote na mateso tunayopitia ameshatangaza kwamba tunao uzima tele ni sisi kumkubali tu na kumkaribisha aje afanye mageuzi (mabadiliko)katika maisha yetu. Mkubali Yesu leo nawe upate burudiko na penzi la kweli lisilo na mawaa.

TUWE NA KIU YA NENO LA MUNGU KWANI NENO NDIO SILAHA YETU KUU, NA TUSOME NENO KWA BIDII BILA KUCHOKA.

Utukufu ni kwa Bwana

Soma hii itakutia moyo.

Am I welcome at your office?


I am leaving   Loveness's office now and I have left blessings, am I welcome in yours?
Receive me with love and send me to other offices/ houses so I can bless them.
Have a blessed day.
I am at the door, I knock. If someone hears my voice and opens the door, I will come in and eat with them at their table. Now He is walking to your house. Let Him bless you and send Him to someone else's house

Yesu anabisha mlango jamani tumfungulie aingie ndani ya maisha yetu abadili kila jambo atusafishe kwa damu yake tuwe safi na tuweze kuishi maisha ya furaha na amani siku zote za maisha yetu kwani bila yeye ufalme wa mbinguni hatuwezi kuuona. Katika Yohana 10:9 atatuambia hivi, MIMI NDIMI MLANGO MTU AKIINGIA KWA MIMI ATAOKOKA ATAINGIA NA KUTOKA NAYE ATAPATA MALISHO. Na pia Kwenye Yohana 14:6 anasema MIMI NDIMI NJIA NA KWELI NA UZIMA, MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI.
Yuko mlangoni mfungulie aingine afanye badiliko la kweli ndani ya maisha yako, usifanye shingo yako kuwa ngumu mwache atende mpokee awe Bwana na Mokozi wa maisha yako nawe hautajuta hata siku moja.

Asante sana Loveness kwa kunitumia, Mungu akubariki mpendwa.